Functions
Usajili wa akaunti
Mafunzo ya kielektroniki yanayotolewa na ESPE, mafunzo ya kimataifa ya kielektroniki mtaala wa magonjwa ya vichochea (homoni) na kisukari kwa watoto
- Mafunzo shirikishi kwa ajili ya kujitathmini na kufundisha darasani
- Kutoa habari za kielimu za kisasa
- Mabingwa wengi wa dunia nzima wamechangia katika kuandika na kupitia yaliyomo
- Ni bure na inawezakupatikana dunia nzima kwa kutumia simu za rununu (mobile)
Anza usajili wako kwa kubofya kuingia - LOGIN
Chagua “ kusajili akaunti mpya”
The kiungo (link) kitafungua fomu
- Jaza fomu
- Chagua jina la kutumia (Username ) mfano : anwani yako ya barua pepe pamoja na “nenosiri”. Zinaruhusiwa alama: -Z a-z 0-9 _.+?#-*@!$%~/:;
- Tafadhali ihifadhi na/au iandike mahali, utaihitaji kila unapoingia kwenye mtandao
- Kubali masharti ya huduma
- Andika herufi na alama za picha kwenye sehemu ya “kuthibitisha mtumiaji”. Kama huwezi kuzisoma vizuri, bonyeza mshale ya kijani kuleta picha nyingine.
- Bonyeza jiandikishe
- Fungua barua pepe ambayo imetumwa kwenye barua pepe (inbox) yako na mfumo ulio-otomatiki
Mfano wa barua pepe itakayotumwa kwako
Kiungo (link) itakuelekeza kwenda kwenye skrini ya kuingia tena: tumia jina lako unalotumia na nenosiri ulilochagua wakati unajaza fomu ya kuomba uingiaji.